Nyota
wa muziki wa kizazi kipya kutoka ‘kruu’ ya Tip Top Connection yenye
maskani yake pande za Manzese jijini Dar es Salaam Abdul Abubakar
Chende ‘Dogo Janja’ ametupiwa virago ndani ya kundi hilo.
Chuma Blog
kiongozi wa kundi hilo
Hamad Ally ‘Madii’ amesema kuwa Dogo Janja ameshindwa kuendana na
makubaliano halisi yaliyokuwepo baina yake na uongozi wa kundi hilo
ikiwemo kuhudhuria shuleni kama alivyokuwa akitakiwa kufanya kila
siku badala yake amekuwa akiendekeza starehe na wakati mwingine
kufanya mambo ambayo kwa namna moja ama nyingine yalikuwa yanalichafua
kundi hilo.
“Tumemkabidhi kwa kaka yake mapema leo tukiwa maeneo ya Ubungo
tayari kwa safari ya kurudi kwao na wakati huo tulifanya mawasiliano
na baba yake kumuarifu kuwa Tip Top hatuko na mwanae kwa sasa”
alisema Madii
Katika hatua nyingine Madii amesema kuwa Dogo Janja alilewa sifa
na kujisahau kufanya yale anayotakiwa kufanya ndani nanje ya kundi
kufuatia mafanikio ya muziki aliyoyapata akiwa na Tip Top Connection
kwani hivi karibuni alitega shule na kwenda kujificha nyumbani kwa
TundaMan hukua akimuaga Madii kuwa anakwenda shule.
Kuona hivyo TundaMan aliamaua kumuarifu Madii na mara moja
kiongozi huyo wa kundi aliamua kwenda kumsaka, lakini baada ya dogo
Janja kugundua kuwa Madii anakuja aliamua kukimbia na kwenda kujificha
uchochoroni lakini akiwa huko mafichoni bahati mabaya alikanyaga kuku
na siri yake kujulikana kuwa amejificha hapao ndipo alipokamatwa na
kuamriwa kufungasha kilicho chake tayari kurejea ‘kileji’.
"vimekuwa ni vitendo vya kila mara kukacha kuhudhuria shule, tumechoka na hatukuwa na njia nyingine ya kufanya alisema Madii'
….Stori by Dismas Ten……
Chuma Blog
ACHENI USHABIKIWA KUEGEMEA UPANDE MOJA MADEE AMEMTESA HUYU DOGO SANA NA KUMTUMIA KIMASLAHI YAKE DOGO KAJANJAUKA WANAMFUKUZA...DOGO RUDI ARUSHA MAANA HUKU NDO HIP HOP NA UTAZID KUTOKA
ReplyDelete