
Baada
ya ukimya wa muda mrefu hatimaye mkali kutoka gemu ya muziki wa
Kizazi kipya Bongo Salum Mohamed ‘Sam wa Ukweli’ anatarajia kutoka na
albamu mpya aliyoibatiza jina la ‘ Hisia Zangu’.
Sam amefunguka kuwa ukimya uliokuwepo ulitokana
na kubanwa na majukumu ya kifamilia na ukosefu wa menejimenti wakati
alipokuwa akitoka kwa mara ya kwanza .
“Ulikuwa ni wakati mgumu kwangu kwa sababu sikuwa na menejimenti
wakati ninatoka mara ya kwanza hivyo nilijikuta kwenye majukumu mengi
hasa baada ya kuoa, hata hivyo nashukuru kuwa nimepeta menejimenti
na tayari niko kwenye harakati za kugonga ‘kichupa kipya’ tayari kwa
mtoko wa albamu yangu niliyoibatiza jina la ‘Hisia zangu’ na singo ya
kwanza kutoka itakuwa ni ‘Najua’ ambayo ndani yake nimejaribu
kuzungumza juu ya wale wanaodhani kuwa bila wao mambo mengine
hayaendi” alisema Sam wa Ukweli
Katika hatua nyingine Sam amedokeza kuwa hakuna ukweli wa aina
yoyote juu ya tetesi zilizoenea mtaani kuwa amefulia kimuziki , huku
pia akitupilia mbali tetesi kua alichanua kwenye gemu kwa kuwa alikuwa
akitungiwa mashairi.
“Mimi sijawahi kutungiwa mashairi , na siyo kweli kwamba
nimefulia ni mipango tu lakini napenda kusema kuwa huu ni wakati
wangu wa kuwaziba midomo waliokuwa wakinishambulia” alisema Sam.
No comments:
Post a Comment