Friday, January 20, 2012

NAPENDA KUSAIDIA CHIPUKIZI LAKINI HAWANA HESHIMA


NYOTA wa filamu ndani ya bongo movie, ambaye ni msanii wa muziki wa kizazi kipya Hemed Suleiman ‘Hemed’, amesema anapenda kuwasaidia wasanii chipukizi lakini wote aliowasaidia hawana shukrani huku wengine wakimtolea maneno ya dharau baada ya kufanikiwa.
Alisema mara nyingi amekuwa akifanya kazi na vijana chipukizi ingawa wote baada ya kuwa na majina kidogo wanashindwa hata kumkumbuka.
Alisema kuwa hadi hapo alipo sasa ameshawatoa nyota kibao ambao wanafanya vizuri katika muziki kizazi kipya pamoja filamu ingawa hakutaka kuwataka majina kwa kile alichodai kuwa hana tabia ya kuwazungumzia kwenye vyombo vya habari.
“Mimi ni nyota mkubwa hivyo jukumu langu hasa kwa vijana wenye uwezo ni kuwasaidia lakini wengi ambao tayari wametoka kupitia jina langu hawana shukrani kwani hata ninapokutana nao mtaani hawataki kunipa salamu,” alisema.

Hata hivyo
Hemed, aliongeza kuwa anatarajia kuachia wimbo wake mpya ambao bado upo studio hivi sasa ingawa umefikia katika hatua za mwisho za kwenda sokoni.

No comments:

Post a Comment