Friday, January 20, 2012

LUCY KOMBA AFURAHISHWA NA KANUNI MPYA KUTOKA BODI YA UKAGUZI


Lucy akiwa katika pose
MWANADADA mtayarishaji na mwigizaji katika tasnia ya filamu Bongo, Lucy Komba, hana tatizo na kanuni zinazotarajiwa kuanza kufanya kazi hivi karibuni ambazo zimetangazwa na Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania, kwani anaamini kuwepo kwa kanuni hizo kutaongeza ulinzi wa kazi zao.
“Binafsi sina tatizo na kanuni hizo, hata hiyo gharama ya kulipia kibali kwa ajili ya kurekodi filamu endapo tu kutakuwa na ulinzi wa kazi zetu. Lakini jambo lingine ni kwamba, inaweza kusaidia kupunguza utitiri wa filamu sokoni, maana filamu zitakuwa chache jambo ambalo litatufanya tuuze kazi zetu kwa muda mrefu,” alisema Lucy.
Baadhi ya wasanii wanalalamika kuwa gharama ya kulipia kibali kwa ajili ya kurekodi ya Tshs. 500,000 ni kubwa huku wengine wakilaumu kuhusu kanuni ndogo ndogo kutoka Bodi ya Filamu.

No comments:

Post a Comment