Monday, June 4, 2012

"Baraja" Msanii aliyegeuka ‘ombamba’ baada ya kumzingua Lamar

Chuma Blog

Utapata picha gani pale msanii uliyemuona kwenye video kali iliyotengenezwa na Karabani huku mashairi yake yakielea juu ya mdundo ‘heavy’ wa mpishi Lamar, akisimamisha gari lako na kukuomba umsaidie mia tano akauone wa mchana (akale)? Surprise bila shaka!
Na kama ndio ulikuwa na ndoto za kujaribu bahati kwenye muziki, ndoto hiyo inaweza kuyeyuka kama glucose mdomoni.
Situation hii imemtokea kwa kijana aitwaye Baraja. Lamar aligundua kipaji chake na kujitolea kumsaidia kwa kumfanyia ngoma bure! Baraja kijana kutoka Shinyanga alikuja Dar kama ombaomba na katika pitapita akaligusa sikio la Lamar ambaye alimsaidia kurekodi wimbo uitwao ‘Maumivu.’
Lamar hakuishia hapo, aliamua kuingia mfukoni mwake na kuchomoa laki kadhaa kumlipia video kwa Karabani.

Mwisho wake ni sad story! Baada ya airtime kadhaa kwenye radio na kwenye TV, dogo si akajiona supastaa! Lamar atamwambia nini wakati mtaani wanamwambia wameiona video yake inabang na wanamkubali kinoma!
“Anasema mimi namdhulumu pesa zake, eti naenda kuperfom nyimbo yake kwenye matamasha!” Lamar alitweet kujibu swali la Bongo5 kuhusu issue hiyo.
Producer huyo mwenye umri mdogo na ambaye anachukua credits za kumrudisha Mr.Nice kwenye game, aliona isiwe tabu na kusitisha umeneja kwa Baraja.

Mpaka unaisoma story hii ni kwamba Baraja mwenye miaka 15, sasa hivi yupo mitaa ya Dar es Salaam akitembeza bakuli kuomba chochote ili amhudumie bosi tumbo, shughuli iliyomleta Dar.

No comments:

Post a Comment