Jacqueline Wolpe |
Amber Rose |
MUONEKANO mpya wa staa wa filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Masawe unaomfanya kufanana ‘kopiraiti’ na modo ‘chakaramu’ wa Kimarekani, Amber Rose kuanzia umbile, pozi tata na unyoaji wa nywele na kubaki kipara, umezua gumzo na sasa anang’ang’aniwa na msala wa picha za utupu.
Wolper amebandikwa jina la Amber Rose wa Bongo kufuatia ‘laifu staili’ yake kufanana na ile ya Amber orijino mwenye sifa kuu ya kupiga picha za utupu na kuziuza kwenye majarida na mitandao ya ‘mambele’.
SIYO KUNYOA TU
“Watu wanazungumzia kunyoa tu kwa sababu ndicho kinachoonekana kwa haraka. Ukweli ni kwamba ukimchunguza kwa ukaribu utagundua vitu anavyofanya vinafanana sana na Amber.
“Hata ukiingia mtandaoni, watu wakimuona Amber akiwa kwenye pozi za utupu mawazo yao yanakimbilia kwa Wolper kwa sababu wanafanana kwa sasa.
HOFU
“Hofu iliyotanda ni kwamba kama Wolper atakuwa anamuiga Amber kwa kila kitu, basi kuna uwezekano naye akaingia kwenye mkumbo huo wa kupiga picha za utupu ili kujiongezea kipato na matokeo yake atapoteza heshima mbele ya jamii kwani kupiga picha za utupu ni aibu kubwa.
“Kusema kweli Wolper ni muigizaji mkali lakini sasa anaweza kuchafuka kwa sababu ya Amber anayejulikana kuwa ni mcharuko,” kilisema chanzo chetu.
Katika kuperuzi na kudadisi, katika picha mpya za Wolper, anaonekana akiwa kwenye pozi tofauti kama ambavyo hupendelea kupozi Amber ambaye kwa sasa ni mpenzi wa mwanamuziki Wiz Khalifa baada ya kutemana na Kanye West, wote wa Marekani.
WOLPER ANASEMAJE?
Baada ya kujiridhisha na maelezo ya watu tofauti wakiwemo rafiki zake wa karibu, Wolper na kumsomea msala wake; ambapo alikuwa na haya ya kusema:
“Hata kama nimefanana na Amber, nitabaki kuwa mimi na hata siku moja siwezi kupiga picha za utupu.”
Mwandishi. Brighton Masalu
No comments:
Post a Comment