Monday, June 4, 2012

Fid Style Friday ndani ya TV mwezi ujao

Chuma Blog
Posted on by Editor

Wewe ni mmoja wa watu waliokuwa wakijiuliza mbona Fid Q hatoi tena episodes mpya za show yake ya online iliyokuwa imejipatia umaarufu ya Fid Style Friday?

Baada ya Chuma kuongea na Ngosha alisema anakuja na njia rahisi zaidi ya kuwafikia watazamaji wengi kwa wakati mmoja.
Baada ya maoni na ushauri mwingi kutoka kwa mashabiki, idea ya kuipeleka show hiyo kali kwa michano, imemuingia vema Fid. Na sasa huenda ikaanza kuonekana kupitia kituo kimojawapo cha runinga nchini.
Fareed Kubanda ametoa taarifa hiyo jana kupitia #AskFidQ ya Twitter baada ya kushauriwa tena na miongoni mwa followers wake kuhusu kuitafutia nafasi show hiyo kwenye TV na si online pekee ambako hutazamwa na watu wenye access na internet tu.

“Show inaitwa #FidstyLeFriday hewani july,” alijibu Fid.
Habari ndio hiyo, Fid Style Friday iliyochini ya Cheusi Dawa Entertainment, itakujia mwezi ujao kwenye kituo cha runinga cha nyumbani. Haijulikani hata hivyo ni kituo gani alichofanya mazungumzo nacho.
Katika kipindi hicho Fid huwatembelea mamc, kwa kila wiki na mmoja ambapo hupiga story na wao wakichana mistari kadhaa.
Miongoni mwa rappers waliowahi kushiriki kwenye kipindi hicho ni pamoja na Nikki Mbishi, One the Incredible, Stereo, Langa, Zaiid, Abbas Kubaff na wengine.

No comments:

Post a Comment