Kwa mujibu wa mtandao wa starcount.com, leo Judith Wambura aka Lady Jaydee ni mtu wa tatu maarufu zaidi nchini Tanzania kwenye mitandao ya kijamii.
Mtandao huo uliozinduliwa rasmi juzi (May 31) ni mkubwa zaidi wa aina
hiyo wenye uwezo wa kusoma tabia za watu bilioni 1.5 duniani kote.
Charts hizo zinajumuisha mambo yote kuanzia makampuni, wanamichezo,
wanamuziki, vyombo vya habari n.k na kuviweka pamoja kwenye chart ambayo
hubadilika kila siku.
Kwa leo Jaydee amekamata pia nafasi ya 34 kwa umaarufu mtandaoni kwa
upande wa Afrika Mashariki na kwa dunia nzima amekamata nafasi ya
19,062.
Katika chart hiyo upande wa Tanzania nafasi ya
pili imekamatwa
Hasheem Thabeet
(3) Lady
Jaydee
(4) mtandao wa Jamii Forums,
(5) Mwananchi
Communications,
(6) Rais Jakaya Kikwete,
(7) Air Tanzania,
(8) ZanAir,
(9) Michael Mlingwa,
(10) Muhidin Issa Michuzi
No comments:
Post a Comment