Thursday, May 24, 2012

FFU jino kwa jino na wakameroon 5,000 wanaoishi Ujerumani

Chuma Blog
Stuttgart,Germany.

Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU,
inatarajiwa kupanda jukwaani siku ya jumamosi mjini Stuttgart,Ujerumani kutumbuiza
katika sherehe ya siku ya taifa la Cameron.kikosi kazi cha Ngoma Africa band aka FFU,
watatingisha jukwaa katika ukumbi wa Arena la  Sportpark Feuerbach, uliopo mtaa 
(Triebweg 85, 70469 Stuttgart) ,Wakameron wapatao 5,000 wanaoishi ujerumani pamoja
na maelfu ya wapenzi wa muziki nchini Ujeruamani watajimwaga uwanjani kupata burudani
kamili kutoka kwa kikosi kazi Ngoma Africa band aka FFU chini ya uongozi wake kamanda
Ras makunja wa FFU,
Ngoma Africa sasa wanatamba na wimbo mpya "Uhuru wa Habari" ambao unasikika hapa
http://www.ngoma-africa.com  au www.ngoma-africa.com

1 comment:

  1. Wakuu wa gwaride Ngoma Africa Band aka ffu aka wana wa mbwa

    ReplyDelete