Tuesday, October 11, 2011

Mr Flavor kutikisa jukwaa la Bongo Stars Search Second Chance

MR FLAVOR
MSANIII wa muziki kutoka nchini NIGERIA  N’ABANIA maarufu kama MR FLAVOR
anayetamba na kibao chake cha ASHAWOO katika vituo mbali mbali vya redio
nchini atawasili leo nchini saaa tano usiku akitokea nchini NIGERIA
tayari kwa kutoa burudani katika fainali za shindano la BONGO STARS
SEARCH SECEOND CHANCE litakalofanyika tarehe 14 mwezi huuu katika ukumbi
wa DIAMOND JUBILEE.

Mkurugenzi wa BENCHMARK PRODUCTIONS ambao ndio waratibu wa shindano hilo
RITHA PAULSEN amesema maandalizi yamekamilika ya onyesho hilo ambapo
wanatarajia msaniii huyo kuwasili usiku ambapo alhamisi atazungumza na
wanahabari.

RITHA amesema kuwa washiriki wannne tu ndio watakaochuana vikali katika
kumsaka mshindi wa shindano hilo atakayejinyakulia shilingi milioni 40,
mshindi wa pili milioni 10 na mshindi wa tatu milioni 5.

Tiketi za onyesho hilo zimeanza  tarehe  ambapo zinapatikana  katika
vituo vya ,maduka ya SHEAR ILUUSION,BEUTY POINT,BIG RESPECT
KARIAKOO,MANYWELE ENTERETIMENT,STEEERS na DIAMOND JUBILEE.

Amewataja washiriki hao ni pamoja na WAZIRI SALUMU  MWENYE NAMBA BSS
23,ROGERS LUCAS BSS 27,BELA KOMBO BSS 05 na HAJI RAMADHANI BSS 11.

No comments:

Post a Comment