Thursday, June 14, 2012

Sauda Mwilima afiwa na mtoto wake

Chuma Blog 

Mtangazaji wa kipindi cha Bongo Beats cha Star TV amefiwa na mtoto wake wa kiume muda mfupi baada ya kujifungua.

Kwa mujibu wa website ya Diamond, Sauda alijifungua mtoto  huyo juzi kuamkia jana katika hospitali ya Kinondoni kwa Doctor Mvungi lakini wa bahati mbaya mtoto wake alifariki dunia.

Hata hivyo mtandao huo umedai kuwa  Sauda bado yupo hospitali na afya yake inaendelea vizuri.

Mwezi April mwaka huu, mtangazaji huyo alifunga pingu za maisha na Kauli Juma, katika harusi iliyohudhuriwa na mastaa.

  CHUMA BLOG inampa pole Sauda Mwilima kwa kupoteza mtoto.

No comments:

Post a Comment