Akizungumza na mtangazaji machachari Adella Tillya maarufu kama (Coco-Toto la mzee tillya) katika kipicha maarufu cha 5SECTION kinachorushwa na Abood Television (ATV) mjini morogoro, mwanamziki Dully Sykes alisema kuwa yeye kama Dully hakatazi mtu yeyote kuchoma nyimbo zake na kuwauzia watu kwani anapofanya hivyo anamtangaza Dully, hivyo ruksa kwa wachoma CD wote ila kwa nyimbo zake tuu kwani hana mpango wa kutoa albam. dully alienda mbali na kusema kuwa hao wanao copy kazi zake wanamtangaza na kumfanya ajulikane zaidi na kupata shoo sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi hivyo kujipatia kipato na maisha kusonga. dully pia aliwaasa wanamziki wa Bongo Flava kusoma alama za nyakati ili kujua mashabiki wanataka nini wakati huu  hivyo kumfanya mwanamziki kuwa juu siku zote kama yeye. Dully aliendelea kutamba kuwa yeye ndie baba wa mziki wa Bongo Flava na ataendelea kuwa juu siku zote na kusema kuwa watashindana lakini hawatashinda.
 

No comments:
Post a Comment