Chuma Blog
Rais
wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi Adrian Nyangamalle (Kulia) akisisitiza
jambo kwenye mwendelezo wa vikao vya maandalizi ya kampeni ya kulipamba
taifa na Sanaa za nyumbani vinavyofanyika Ukumbi wa BASATA.
Katikati ni Katibu Mtendaji wa BASATA Ghonche Materego na Katibu wa
shirikisho hilo Godfrey Ndimbo.
Katibu Mtendaji wa BASATA Bw.
Materego akiongea na wajumbe wa Kamati ya kundaa kampeni ya Kulipamba
taifa na Sanaa za nyumbani (hawako pichani) inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Mmoja wa wajumbe wa kamati ya Kulipamba taifa na Sanaa za nyumbani Fred Halla.
Na Mwandishi Wetu
Wadau mbalimbali nchini hususani viongozi wa kitaifa na kidini,
wanasiasa na wamiliki wa majengo mbalimbali nchini wameombwa kuunga
mkono kampeni ya
kulipamba taifa na kazi za Sanaa za kitanzaia inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
kulipamba taifa na kazi za Sanaa za kitanzaia inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Akizungumza katikati ya wiki hii kwenye mwendelezo wa vikao vya
maandalizi ya kampeni hiyo Rais wa Shirikisho la Sanaa za Ufundi nchini
Adrian Nyangamalle
alisema kuwa uungwaji mkono wa wadau hao utalifanya taifa kupendeza na kuwa kivutio kwa kila mtu.
alisema kuwa uungwaji mkono wa wadau hao utalifanya taifa kupendeza na kuwa kivutio kwa kila mtu.
“Tunategemea kwa kiwango kikubwa uungwaji mkono kutoka kwa wadau hasa
viongozi wetu wa kitaifa, lengo ni kumfanya kila mtanzania aone fahari
kwa kupamba
na Sanaa za nyumbani lakini pia afurahie mandhari nzuri ya taifa lake” alisema Nyangamalle.
na Sanaa za nyumbani lakini pia afurahie mandhari nzuri ya taifa lake” alisema Nyangamalle.
Kwa mujibu wa Nyangamalle, Tanzania imejaaliwa Sanaa nyingi za mikono
kama za vinyago na michoro, zina mvuto wa aina yake, zinavuta wageni
wengi kuja
kuzitazama hivyo kuzipamba kwenye maeneo yetu ya wazi na maofisi kutabadili kabisa muonekano wa miji na ofisi zetu.
kuzitazama hivyo kuzipamba kwenye maeneo yetu ya wazi na maofisi kutabadili kabisa muonekano wa miji na ofisi zetu.
“Tunalenga kampeni hii isambae, ifike mahali iwe lazima kwa ofisi
zetu za umma na maeneo ya wazi kupambwa na Sanaa za mikono kutoka
nyumbani. Ni wazi
viongozi wetu wakiunga mkono tutaleta mabadiliko” alisisitiza Nyangamalle.
viongozi wetu wakiunga mkono tutaleta mabadiliko” alisisitiza Nyangamalle.
Kuhusu mikakati ya uzinduzi wa kampeni hiyo Rais huyo mwenye dhamana
na Sanaa za mikono nchini alisema kuwa, inaendelea vizuri na kwa hatua
za mwanzo
itahusisha maonesho ya Sanaa za kupamba maofisini sambamba na kushawishi watendaji maofisini kununua kazi hizo za mikono.
itahusisha maonesho ya Sanaa za kupamba maofisini sambamba na kushawishi watendaji maofisini kununua kazi hizo za mikono.
“Bado hatujapanga kalenda rasmi ya uzinduzi wa kampeni hii lakini
mikakati inaendelea vizuri, wito wangu ni kuomba viongozi wetu wa juu na
watanzania kuona
umuhimu wa kampeni hii” alimalizia Nyangamalle.
umuhimu wa kampeni hii” alimalizia Nyangamalle.
No comments:
Post a Comment