Chuma Blog
NA MDAU WETU, ZANZIBAR
MSHIRIKI WA KWANZA KUFIKA KWENYE USAHILI NGOME KONGWE, SALMA YUSUF AKIWEKA GUITAR YAKE
MSHRIKI TOKA DODOMA, DAYNA BROWN AKIJARIBU KWA MARA YA PILI HUKU ZANZIBAR.
WASHIRIKI WAKIFANYA MAZOEZI YA KUIMBA KABLA YA KWENDA KWA MAJAJI
MSURURU WA WASHIRIKI WAKIFANYA USAJILI KWA AJILI YA EPIQ BONGO STAR SEARCH
MSHIRIKI NAMBA 00775 AKIPOKEA NAMBA ZA USHIRIKI |
WASHIRIKI HAO WALIOJITOKEZA KWA KATIKA
USAILI HUO UNAOFANYIKA NCHI NZIMA CHINI YA MADAM RITA, SALAMA NA MASTER
J, WALIWALALAMIKIA MASTER J NA SALAMA KUWA NI KIKWAZO KIKUBWA KWA
WASANII WENGI WANAOINGIA KATIKA KINYANG'ANYIRO HICHO KUJARIBU BAHATI
YAO.
WALISEMA MASTER J NA SALAMA WAMEKUWA WAKIWAKATISHA TAMAA WASANII
WENGI NA KUONGEZA KUWA KITENDO HICHO KIMEWAFANYA WENGI KUSHINDWA KUFIKIA
MAFANIKIO YA NDOTO ZAO.
" HAWA JAMAA SIJUI VIPI YANI KILA SIKU WAO KAZI NI KUTUKATISHA TAMAA NA MANENO YAO KASHFA", ALISEMA MMOJA WA WASHRIKI HAO.
KWA UPANDE WAO, MASTER J NA SALAMA WALISEMA KUWA WAO LENGO LAO SIO
KUWAKATISHA TAMAA WASHIRIKI BALI NI KUWAJENGA ILI KUFIKIA MATARIJIO YA
MASHINDANO HAYO.
" UNAJUA SISI TUNAFANYA HIVYO ILI KUWASAIDIA, HAMNA ASIYEJUA KWAMBA
MUDA NDIO KITU PEKEE DUNIANI AMBAYO IKISHAPOTEA HAIWEZI KUJIRUDIA, MUDA
UKIENDA UMEENDA, KWA SIONI SABABU YA MTU KULAZIMISHA FANI," ALISEMA
MASTER J.
TIMU HIYO INAZUNGUKA MIKOANI KUSAKA WASHIRIKI WATAKAOINGIA KATIKA 50
BORA YA MASHINDANO HAYO AMBAYO YANADHAMINIWA NA ZANTEL KUPITIA EPIQ
BONGO.
No comments:
Post a Comment