Chuma Blog
Katika hali inayoashiria kuwa mwanamuziki wa kike nchini
Tanzania Sarah Kaisi aka Shaa ameipuzia habari ya gazeti la udaku la Uwazi kuwa
wameachana na mpenzi wake wa zamani Master J, ameliscan na kuliweka Twitter.
Shaa |
Gazeti
hilo lililotoka (June 5) lina kichwa cha habari kisemacho "Master
Jay & Shaa wamwagana. Babu Tale atajwa kuwa chanzo, Master Jay
aelezea kilichotokea."
Akiwa amemkopi @masterjtz , Shaa ameandika “Woke up to
this...cute! For show bookings,interviews and all plz contact Babu Tale.”
Master Jay |
Gazeti la uwazi linasema wapenzi hao wameachana kisa Babu Tale.
Hata hivyo Shaa ameendelea kusisitiza juu ya watu wanaotaka kufanya show naye wawasiliane
na Tale ambaye inavyoonekana ni meneja wake.
Babu Tale |
Wakati Master Jay yuko busy na EpiqBSS, snitches wako busy kuiangalia
‘Siri ya Penzi’ kati yake na Shaa.
No comments:
Post a Comment