Chuma Blog
Diamond mapema jana akiwa katika studio za Clouds FM kwa ajili ya interview.
Diamond
aliulizwa ni kwa vipi aliweza kujielezea vizuri sana kwa lugha ya
Kingereza baada ya performance yake kwenye Big Brother StarGame maana
wengi huwa wanashindwa ifikapo hatua hiyo Diamond alifunguka na kukiri
kwamba mrembo Wema Sepetu amechangia kiasi kikubwa kwake kujua lugha
hiyo na kusema napenda kumshukuru 'WEMA ENGLISH COURSE'......
kusema ukweli nilifurahi sana kusikia hivyo maana pamoja na mascandal
yao yote angalau Diamond ameweza kuongelea upande mzuri wa Wema na ni
jinisi gani ameweza kuchangia mafanikio yake kwa kiasi flani.
Wakati
huo huo Diamond pia ameongela tour yake ambayo anatarajia kuifanya
nchini Marekani baadae mwaka huu na nyumba anyo jenga Tegeta ambayo
amekiri mpaka sasa ametumia karibia Tshs milioni 69. Nyumba ni ya
kisasa, ina vyumba vya kulala vinne, vitatu vyote master, kuna studio,
jiko, choo, bafu nk. Pamoja na nyumba hiyo kuna zingine pia ambazo
hakupenda kuongelea ila I hope and I'm sure kuna siku atafunguka.
No comments:
Post a Comment