Chuma Blog
May na
June imekuwa miezi yenye habari njema kwa kundi la Hip Hop la nchini Kenya,
Campmulla.
Mwezi uliopita
kundi hilo lilitajwa kuwania tuzo za BET katika kipengele cha Best
International Act Africa, na sasa vijana hao watano wamekamata deal nono kutoka
kwa Universal Music Group.
Mkataba huo
uliosainiwa nchini Afrika Kusini unawafanya wawe label moja na P-Square wa
Nigeria ambao nao walisaini mkataba huo wiki hii.
Campmulla wakati wa shughuli ya kusaini mkataba |
Nao pia
kama Peter na Paul Okoye, wamejiunga na label iliyo na wasanii zaidi ya 100
duniani. Miongoni mwa wasanii wakubwa waliochini ama waliowahi kuwa chini ya
UMG ni pamoja na Young Jeezy, Wale, William, Tyga, Soulja Boy, Shania Twaim,
Shantele, Steve Wonder, Akon, Rick Ross na Rihanna.
Wengine ni
Nicki Minaj, Ne-yo, Nas, Melanie Fiona, Madonna, Lil Wayne, Keri Hilson, Kanye
West, Justine Bieber, Jennifer Lopez, Drake, Dr. Dre na wengine wengi.
Makao
makuu ya UMG yapo Santa Monica, California nchini Marekani lakini ina matawi yake
sehemu mbalimbali duniani kote.
No comments:
Post a Comment