Wednesday, June 6, 2012

GODZILA ASIMAMA MUZIKI KWA MUDA



Chuma Blog
Mwanamuziki toka pande za Salasala, The King of Salasala, Godzila, hatopanda jukwaani tena mpaka apone kidonda kilichoshonwa nyuzi.
Godzila alisema alipata  ajali  wakati akitoka Mikocheni kwenda Studio, na punde tu walipofika njiani Coaster moja, ilikuja na kuwagonga kwa nyuma kiasi cha  kujigonga na kuchanika sehemu ya mdomoni.
Amesema baada ya tukio hilo ilimbidi afike hospitali na kushonwa nyuzi mbili, ambazo hadi sasa bado anafuatilia matibabu.
Hivyo amesema hatuweza kupanda jukwaani mpaka hali yake itakapotengemaa na kuwa sawia ndipo ataingia tena mzigoni kwa ajili ya burudani zaidi.

No comments:

Post a Comment