Wiki hii Prezzo ameachia ngoma iitwayo The Greatest ambayo
amemdiss Jaguar kitu kinachoashiria kuwa beef hii haijaisha.
Tungependa kukupa
nafasi ya kusikiliza interview walizowahi kufanyiwa na Capital Fm kuhusiana na
beef yao.
Katika interview ya Jaguar na radio hiyo maarufu nchini
Kenya Jaguar aliongea mengi ya kumponda Prezzo.
Alizungumza kuwa anamshangaa
Prezzo kujidai kuwa anavyaa bling bling wakati akipanda kwenye stage watu
wanamzomea.
Jaguar aliendelea
kujinadi kuwa yeye sasa hivi ananunua
ardhi wakati Prezzo anauza na kuwa hizo Gucci ambazo Prezzo hujisikia
kwenye
nyimbo ni fake ama za mtumba na anajua wapi huzinunulia na kuongeza kuwa
rais huyo wa CMB yuko broke kiasi cha kushindwa kuwanunulia hata pombe
washkaji.
Jaguar alisema pia kuwa yeye hutoa mkopo wa fedha hivyo kama
Prezzo akihitaji anamkaribisha.
No comments:
Post a Comment