Chuma Blog
Kwa muda mrefu sana Hermy B, CEO
wa B’Hits Music Group na Ambwene Yesaya aka AY walikuwa maswahiba zaidi ya
chanda na pete.

Uhusiano wao ulikuwa na mafanikio kwa kila mmoja. Nyimbo kama
habari ndio hiyo, nangojea ageuke, Leo, Bed and Breakfast na nyingine nyingi
zake AY zilitengenezwa ba Hermy B ambaye pia ni jaji wa mashindano ya Tusker
Project Fame.
Kabla ya nyimbo hizo ni wachache sana waliokuwa wanamjua Hermy B.
Ni wazi kuwa AY alimtambulisha Hermy kama miongoni mwa watayarishaji wazuri
nchini Tanzania.
Lakini hivi karibuni kumekuwepo na
fununu kuwa ushkaji kati ya nguli hao umefikia tamati. Tweet hii iliyoulizwa
kwa AY na mdau mkubwa wa leotainment @Haile19 leo (May 23) ikatupa jibu la
maswali yetu kuhusiana na tetesi hizo “ni kweli ur not with #Bhitz anymore!”
ambapo AY amejibu moja kwa moja “YES”
Mashaka kuhusiana na uhusiano wao
yalianza kuonekana baada ya AY kuwa na mpango wa kwenda kufanya video nchini
Afrika Kusini akiwa na producer wa Mj records, Marco Chali ambaye ndiye aliyeutengeneza
wimbo huo. Na jana (May 22) wamewasili mjini Johannesburg kwa ajili ya shughuli
hiyo.
Wakati wa urafiki kati ya AY na
Hermy hakuna kazi ambayo AY alikuwa akiifanya nje ya usimamimizi wa Hermy.
Uamuzi wake wa kwenda kufanya kazi MJ Records ukaashiria kuwa uhusiano wao
umeingia matatani. Kuna maneno pia sababu za kuvunjika kwa ushkaji huo umetokana
na tamaa ya Hermy B ambaye alidaiwa kumtaka AY aanze kumlipa producer huyo
shilingi milioni 10 kwa wimbo mmoja.

Kwa wengi kitendo hicho kinaonesha
wazi kuwa Hermy alianza kuingiwa na kinyongo na kuona kuwa analipwa kiasi
kidogo licha ya AY kufanya show nyingi ndani na nje ya nchi zinazomlipa sana. Kwa
kawaida kama huo ni ukweli basi Hermy alikuwa sahihi kwamba kwanini umlipe laki
4 ama tano kwa single moja wakati wewe unaingiza zaidi ya milioni 20 kwa wiki
moja ama mbili (makadirio).
Hata hivyo shilingi milioni kumi
kama tozo ya wimbo mmoja kwa Tanzania bado haiwezi kuwaingia akilini wasanii
wengi hata wale wenye kipato kikubwa akiwemo AY.
Sababu nyingine ya wazi kabisa
kuwa AY na Hermy si ‘wana’ tena ni ukaribu wa hivi karibu kati yake na Master J
ambao bila shaka umetokana na uswahiba wa Master J na Salama Jabir ambao nao ulitokana
na kuwa majaji wa Bongo Star Search. Pamoja na kuwa Master J na AY
wanafahamiana tangu siku nyingi kama msanii na producer, tunahisi kuwa
ushirikiano wa AY na Salama Jabir katika kuanzisha kipindi cha TV cha Mkasi
kimewaweka karibu zaidi Master J na AY kwa kupitia Salama.
Sababu ya tatu iliyotufanya
tutilie shaka uhusiano wa B’Hits na AY, ni kile alichokisema Hermy B na kuandikwa
hapa mwanzoni mwa mwezi huu kuwa hakuna msanii tajiri Tanzania.
Kauli hii ya Hermy ilitupa mashaka na kuiona kuwa huenda imetokana na kitu kinachomuumiza moyoni hususan mafanikio ya AY ambaye wengi tunaamini ni miongoni mwa wasanii matajiri nchini Tanzania.

Kauli hii ya Hermy ilitupa mashaka na kuiona kuwa huenda imetokana na kitu kinachomuumiza moyoni hususan mafanikio ya AY ambaye wengi tunaamini ni miongoni mwa wasanii matajiri nchini Tanzania.
Hata kama AY na Hermy B (B’Hits)
wakiendelea kutokokuwa karibu kimuziki, walipofika wote si pa kubeza na
kutokana na ubunifu, kujituma na uwezo wao binafsi kila mmoja ataendelea kupata
mafanikio katika upande wake na maisha yanaendelea
No comments:
Post a Comment