Thursday, May 31, 2012

The Mboni Show ‏kuruka leo kwa mara ya kwanza

Chuma Blog


Ile talk show iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu nchini, The Mboni Show, leo inatarajia kuanza kuruka rasmi kupitia EATV.

Tarehe 25 mwezi huu show hiyo ilizinduliwa rasmi katika hoteli ya Serana na kuhudhuriwa na watu mbalimbali maarufu nchini.
Katika show ya kwanza itakayooneshwa leo, mwanamuziki wa Kenya Wyre ataonekana akihojiwa.
Kupitia akaunti maalum ya Twitter ya show hiyo leo imeandikwa, “Yaaaaaap ni leo saa 3 kamili usiku mpaka saa nne EATV the first show ya THE MBONI SHOW ndo mpango mzimaaaa kutana na Wyre akielezea CHUKI.”
The Mboni Show ni kipindi cha TV chenye lengo la kuelimisha, kufunza, kuburudisha na kuisaidia jamii ya kitanzania.

No comments:

Post a Comment