Chuma Blog
Tangu mfalme wa rhymes Afande Sele atangaze kuwania ubunge mwaka
2015, amekuwa akiitumia sana Facebook kutoa ujumbe maridhawa wa
mabadiliko.
Alhamis hii rapper huyo ambaye jina lake halisi ni Seleman Msindi
amewashauri wazazi kuwajengea watoto wao msingi wa mapema kuhusu chanzo
cha umaskini nchini.
“Tujenge misingi mpaka kwa watoto wetu kuwa umasikini tulionao,
unaletwa na wachache!! Na hatutaki wala hatupendi kuona wao wakiwa na
maisha mabovu, ndio maana namuonyesha njia sahihi, ili wakati wake
ukifika asihadaike”, ameandika Afande.
Katika ujumbe huo Afande pia amesema, “kuna wakati maamuzi madogo
sana yanaweza badilisha maisha yetu daima!! Hakuna ubaya kuhitaji
mabadiliko, kama yatakua katika njia sahihi.”
Ni mrefu tangu msanii huyo mkongwe aliyetamba na ngoma kama
‘Darubini’ na ‘Mtazamo’ hajahit kwenye radio jambo ambalo limemfanya
avitupie lawama baadhi ya vyombo vya habari kuwa vinauua muziki wa
Tanzania kwa kupendelea wasanii wachache.
No comments:
Post a Comment