Chuma Blog
Mtangazaji wa Clouds FM Loveness aka Diva anatarajia
kujaribu bahati yake kwenye muziki wa Bongo Flava kuona upande huo wananchi watampokeaje.
story hii ni kuwa Diva huyo atamshirikisha pia Diamond kwenye wimbo utakaotengenezwa na Lamar.
Taarifa hizo zimethibitishwa na Diamond mwenyewe kupitia twitter ambapo alikuwa akimjibu mtangazaji wa Radio Citizen na Citizen TV za Kenya, Willy Tuva "Kuna kibao nitafanya na Diva wa Clouds chini ya Fish crab cookout"

Diva ambaye hujiita ‘Mimi’ ni miongoni mwa watangazaji
wanaozungumzwa zaidi nchini kwa mabaya mengi na mazuri machache kutokana na aina ya
utangazaji wake kwenye kipindi cha Ala za roho katika kituo hicho cha radio
maarufu kwa burudani nchini kutokana na sifa yake ya kuongea mambo mazito ya
kimapenzi bila kificho.
Diva anategemea kuachia wimbo utakaojulikana kwa jina la ‘Piga
Simu’ chini ya producer Lamar wa Fish Crub!
Leo (May 24) Lamar ametweet “Diva aka mimi under xclusive
muzik the lebal !soon to release a hit song piga simu.”
Yetu masikio kujua kama Diva atajikusanyia mashabiki pia
katika muziki baada ya kufanya vizuri upande wa radio ama atawatukana tena
wanaume!
Mtangazaji huyo amelazimika kuomba radhi baada ya kusema kwenye kipindi chake kuwa wanaume wa kitanzania ni wachafu,wananuka boxer,midomo,vikwapa n.k.
Mtangazaji huyo amelazimika kuomba radhi baada ya kusema kwenye kipindi chake kuwa wanaume wa kitanzania ni wachafu,wananuka boxer,midomo,vikwapa n.k.
No comments:
Post a Comment