Wakati wapenzi wa muziki wa Tanzania wakiendelea kuijadili
performance ya Diamond jana kwenye Big Brother Eviction day, kuna wengine
waliozitafsiri shukrani zake kwa vyombo vya habari kama za kibaguzi.
Hiyo ni baada ya Diamond kutoa shukrani kwanza kwa Clouds
FM kwa mchango wake kutokana na mafanikio aliyoyapata mpaka kufikia kupanda
kwenye majukwa ya kimataifa.
Baada ya kuandika hivyo, mmoja wa watu wanaomfollow
mwanamuziki huyo kwenye mtandao wa twitter akaandika “inamaana media zingine
hazimpi support Diamond?”
Diamond akiwa Airport Johannesburg asubuhi ya leo akijiandaa kurudi Bongo |
Ili kufafanua Diamond akaandika “nimetweet hiyo coz ni
media inayotoa habari za Bigbrother Africa, usinukuu tofauti kuleta malumbano
tafadhali.”
Naye mtangazaji wa radio hiyo, Hamisi Mandi aka BDozen akafafanua kwa kuandika, “nafikiri hii itakua ni special thanks!!!”
Kuweka mambo sawa zaidi kuhusiana na utata huo Diamond
ametawaka watu wasinukuu tweet zake vibaya ili kuleta malumbano na kuwaomba
wawe positive daima!
Baada ya kuipa kipaumbele Clouds FM, ndipo Diamond
akavikumbuka vyombe vingine vya habari,” shukrani kwa media zingine zotee from Tanzania,
kwa kusaidia kazi za muziki wa watanzania, mbarikiwe.
Baada ya kuiwakilisha vyema Tanzania, Diamond anarejea
leo nchini.
No comments:
Post a Comment