Saturday, March 31, 2012

Diamond Napokea Dola Tuuuuuuuuu....

Chuma Blog
 ...Ehe! utata mkubwa ambao ulizuka ni hapa ambapo mwanadada huyu alimtuza dola za Kimarekani, Diamond
 ...Diamond aliendelea kuimba huku mwanadada huyo akimtunza huku akitoa tabasamu na kicheko
 Mwadada huyo hapa alikuwa amemaliza na kuondoka kwa mikogo..
Baada ya Diamond kurudi stejini ndipo mwanadada Wema Sepetu alienda kumtuza na pesa zake kukataliwa. Wema alikaa akimbembeleza kwa muda wa dakika 10 japo zoezi lake halikufanikiwa.
 ...Diamond aliendelea kuwajibika huku Wema akijaribu kumbembeleza
 Bembeleza, bembeleza na wewe jamaa ndiyo aliendelea kuwajibika
 ...Ndipo alipochukia na kuzitupia hizo hela stejini huku akiondoka huku akiwa amenuna
 ...Shamim Mwasha akilaumu kitendo alichokifanya Diamond cha kukataa hela alizoenda kutuzwa na Wema... 'Haiwezekani hii ni aibu sana'
Pesa alizokataa kuzichukua zikiwa zimetupwa 
 ...Hapa alipiga kitu cha 'Nimpende Nani'
 ...Jokate na marafiki zake wakishangilia
 ...Baada ya tuio hilo kutokea Mange Kimambi alimuita mshereheshaji wa tamasha hilo, Taji Liundi na kumuomba amuite Diamond aje amuombe msamaha na ndipo Diamond akakataa.
 ...Diamond alishuka na kuelekea kwa mwanadada Jokate Mwegelo na kuanza kukata mauno.
 ...mwanadada Mboni Masimba akiwa amevaa t-shirt alizokuwa amevaa.
 ...Aha! nimependeza sana
Taji Liundi akimbembeleza Diamond ili aende nae kwa Wema ndipo Diamond akakataa. 
 
Mwanadada Mariam (Miss Popular) akimfuta jasho Diamond wakati Taji Liundi akimbembeleza ili aende kwa Wema.
 
...Diamond akiserebuka na warembo
 Marafiki wa Wema Sepetu wakijaribu kumbembeleza wakati akimwaga chozi... huku watu wengine wakishangilia na kuimba aibu yetu au aibu yao?
 ...hapa mwanadada akijaribu kubembeleza bila matumaini.
Baada ya Barnaba kuimba wimbo wa 'Napembelezwa' ndipo mwanadada Wema alienda kumtuza na kutoa machungu yake. Kwa mujibu wa uchunguzi na maoni ya watu mbali mbali walikiona kitendo cha Wema Sepetu kwenda mbele kumtuza Diamond ni sawa na kujidhalilisha na kuhusishwa na mambo ya kishirikina.
Pia Justmine Loyce Bobbie alisema: Kwanini Wema anamfatafata mtoto wa watu kila kona? amuache na maisha yake jamani.. mbona Diamond hamfatilii lol, YATAMSHINDA


Picha kwa msaada wa: 
kajunason

1 comment:

  1. toka huko na wewe huyo Diamond wako ndio mshamba

    ReplyDelete