Chuma Blog
![]() |
Dyna, Beatrice, Rachel & Queen. |
Katika kipindi cha Diva Loveness Love wa ALA ZA ROHO Clouds fm... live kwenye show yake alhamis march 29 usiku... huwa kila alhamis moja katika mwezi mmoja show yake ya radio inaungana na Clouds Tv, wasanii wanaalikwa na kuimba Live pamoja na mahojiano.
Waliimba live na kuhojiwa! Beatrice alitokwa na machozi wakati akizungumzia alikotoka na alipo sasa.Kwani alifunguka na kusema, kazi wanazofanya wasanii wengi wa kitanzania,jinsi wanavyochukuliwa kimataifa ni tofauti sana na maisha yao halisia yao.Alisema kwa mfano mimi simu ninazopigiwa toka kenya, burundi nk naonekana ni msanii mwenye mafanikio.Kwani mwaka wote nimefanya show kubwa mbili tu hadi sana.Ila inatia uchungu kwa kweli,nawaomba wadau waangalie maslahi yetu,kwani tunateseka sana" Alisema Beatrice huku akilia kwa uchungu. Kwa upande wake msanii Dareen alionekana kukazia hoja hiyo huku akielekeza kilio chake serikalini.
Wasanii hao wakike ambao ni nominees wa KILI MUSIC AWARD walitoa malalamiko hayo walipoitwa katika studio za clouds fm katika kipindi cha Ala za Roho kinachoendeshwa na mtangazazi loveness love, pia kilirushwa live na kituo cha clouds tv na kuwapa nafasi ya wasanii hao kuomba kura kwa mashabiki ili wawachague katika mashindano ya kili music award 2011-2012.
No comments:
Post a Comment