Friday, January 13, 2012

MAZISHI YA MZEE KIPARA HUKO KIGOGO

Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC) Mh. Samwel Sitta akiwasili katika msiba wa Muigizaji wa siku nyingi Mzee Kipara aliyefariki usiku wa kuamkia juzi huko Kigogo jijini Dar es salaam, Mzee Samwel Sitta ameungana na waigizaji, ndugu jamaa, na marafiki wa marehemu Mzee Kipara ambaye mwili wake umezikwa  katika makaburi ya Kigogo, wanaompokea kulia ni Saimon Mwakifwamba Rais wa Shirikisho la wasanii wa Filamu nchini na kushoto ni Mwigizaji Hashim Kambi.
Nami nilipata picha ya ukumbusho na vijana wangu kutoka kimumeni yaani TMK kulia ni Juma Kassim a.k.a Sir Nature na kushoto ni Rich One ambaye anasema eti "soon nitawakilisha kwenye video yake mpya".
Mmoja wa masheikh akitoa mawaidha katika msiba wa mzee Kipara huko nyumbani kwake Kigogo.
Mzee King Kikii wa pili kutoka kulia naye amehudhuria katika mazishi hayo, kulia kwake ni Juma Mbinzo na kushoto ni Muigizaji Chuzi na Mwanamuziki Malou Stonch.
Senga kushoto na mwenzake Pembe walikuwepo Kumsindikiza mwigizaji mwenzao na mzee wao katika shughuli za uigizaji.
Mzee Magali akikata mkwanja wake wa Mchango kwa mwigizaji Natasha na kulia anayeshuhudia ni Mwigizaji Hashim Kambi.
Cheki Budi naye akiwasili katika msiba huo.
Waigizaji mbalimbali wa kike wakiwasili katika msiba huo.
Mzee Merinyo wa Afrika Sana naye amehudhuria katika mazishi hayo huko Kigogo.
Mwigizaji Cate kulia na wenzake wakiwasili katika msiba huo jioni ya leo huko Kigogo. Mzee Small akiwa amebeba ubao ikiwa ni matayarisho kwa ajili ya mazishi ya Mzee Kipara aliyefariki jana jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment