Sunday, September 18, 2011

MZEE YUSUF APEWA AWARD YA HASHIMA HOLLAND "Jijini Den Haag"


Mzee Yusuf akiendeleza kuwapagawisha mashabiki wake jijini Den Haag.

Hapo mwenye kuramba aliramba kisawasawa,full kujiachia,full mzuka ndani ya Den Haag.

Mzee Yusuf mfalme wa Taarabu Tanzania alitoa zawadi kwa dada aliyependa ukumbini,hapa akimpongeza dada aliyevaa vazi la kiafrika japo yupo ulaya na ndiye mshindi aliyependeza siku hiyo ya jana.


Mzee Yusuf alitoa zawadi kwa mtu aliyependeza ukumbini hapo na alitoa zawadi kwa mtu aliyeweza kucheza vizuri taarabu inavyotakiwa kuchezwa,Pichani ni Mama Sharon akipata picha ya pamoja na Mzee Yusuf mara baada ya kupokea zawadi yake ya mwanadada aliyeweza kucheza vizuri taarabu vile inavyotakiwa kucheza.

Mmoja wa Viongozi wa kampuni ya UWATU akimkabidhi AWARD  Mzee Yusuf kama heshima ya kuweza kufanikisha muziki wa Taarabu nchini Tanzania kukubalika.

Mzee Yusuf akiitazama vyema Award yake huku akitoa maneno ya shukrani kubwa sana kwa mambo mazuri ambayo aliyapata toka kwa wenyeji na waandaji wa show yake.

Mzee Yusuf akipongezwa kwa zawadi yake ya Award ya  heshima kwa kuendeleza vyema muziki wa taarabu nchini Tanzania.Pichani akipata Flash na bidada mrembo kabisa jijini Den Haag.

Acha nijimwaga mieee na Mpenzi wangu miee acha nijimwage mie na mpenzi wangu jamaaaaaaniii!!

Bidada Amina akiwa na Euro 200 mkononi kwa ajili ya kumtunza Mzee Yusuf kwa jinsi alivyowarambisha kisawasawa.
Mzee Yusuf akiwa na mmoja wa Mapromota wa kike nchini Holland,bidada Vicky..Vicky ndiye aliyeongoza shughuli za shughuli zote ukumbini hapo.

Mfalme wa Taarabu Tanzania,Mzee Yusuf akikonga nyoyo za wapenzi wake jijini Den Haag.


Dj aliyekaranga vyombo ipasavyo na kumfanya Mzee Yusuf Kuwarambisha mashabiki kisawasawa,ni Dj Alein.Dj Alein ni Dj anayekubalika nchini Holland.
Kwa picha na habari zaidi: http://magangaone.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment