Tuesday, June 12, 2012

KWANI WASANII WAKUBWA NAO WANA COPY NYIMBO

Chuma Blog

 
  
 Linapokuja suala la kusample wimbo haijalishi kama msanii ni mkubwa ama mdogo watu watasema na ukweli lazima utawekwa wazi. Kwa dunia hii ya leo yenye maendeleo makubwa ya internet ukisample huwezi kujificha na hata ukifanikiwa ipo siku wajanja watagundua tu.
Solothang ndiye aliyeligundua hili na sisi tukaamua kuhakikisha na kukuta kweli Ameen ya MwanaFA ni sample ya wimbo wa Cecile uitwao Hey aliomshirikisha Agent Sasco. Wimbo huu upo kwenye albam yake ya mwaka jana iitwayo Jamaicanization.

Producer wa wimbo huu ambaye ni Dully Sykes amesample wimbo huo kila kitu. Chorus yake mwenyewe Dully ni copy and paste ya chorus ya Cecile. Kipya kwenye Ameen iliyosifiwa sana wiki hii kwa maneno ya maana ya MwanaFA, ni mashairi tu.

Siku zote sampling pamoja na kuwa si jambo baya kihivyo huleta maana mbaya hasa kwa producer ambaye huonekana hana idea kiasi cha kuchukua za wengine.

Sikiliza mwenyewe na useme kama Dully Sykes ameonewa!

No comments:

Post a Comment