
Mbunge  wa Mbeya Mjini (Chadema), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’, ameweka kambi ndani  ya A-Town pamoja na Vinega wote, wakifanya harakati za nguvu,  kuwahamasisha wananchi wajae kwa wingi Uwanja wa Triple A ambako shoo  kali ya Hip Hop itachukua nafasi Desemba 18, 2011 (Jumapili hii).
Sugu amesema kuwa yupo kwenye  mishemishe kibao, akifanya ‘interview’ kutoka redio moja hadi nyingine  za Arusha, kutengeneza uelewa kwa wana wa Arusha kuhusu harakati za Anti  Virus zinavyolenga kumkomboa msanii wa Tanzania.Ni Venega wale wale  wanaosababisha kizaazaa mtaani kwa mix-tape zao za Anti Virus kisha  wakaibua mambo makubwa kwenye Tamasha la Burudani kwa Mashabiki, Muziki  unalipa Uwanja wa Chuo cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama, Dar es Salaam.
Taarifa ni kwamba shoo hiyo ya  Triple A, itaanza saa 8:00 mchana mpaka saa 6:00 usiku.Sugu ndiye  ataongoza shoo hiyo, wakongwe Mabaga Fresh, Big Dog Pose, Hardmad, Zay B  na Sister P, watafanya kieleweke..
Shujaa wa Kundi la Wagosi wa  Kaya, Fred Mariki ‘Mkoloni’, Anselm Ngaiza ‘Soggy Dog’ na mwana Hot Pot  Family mwenzake, Suma G, Mapacha, Dani Msimamo, Rama Dee, Peen Lawyer,  Adili Mkwela ‘Hisabati’, D wa Geto, Magazijuto, Coin Moja, LWP ‘Majitu’  na wengine kibao watakuwepo kuhakikisha wana wa Arusha wanapata burudani  ya ukweli ya Hip Hop.
Mratibu wa shoo hiyo, Mkoloni  alisema kuwa muziki (sound) utakuwa ni wa kiwango cha juu ambao thamani  yake ni shilingi milioni 50.
“Ma-DJ  wenye kiwango cha juu watakuwepo kufanya mambo makubwa. Atakuwepo  mtaalam,Profesa Ludigo. Wasanii watakaokuwepo ni wengi mno,  tutakumbushia mapini ya kitambo na baadaye Vinega watafanya Anti Virus  ieleweke,” alisema Mkoloni.
No comments:
Post a Comment