
Mkali wa muziki wa hip hop kwenye anga ya muziki wa kizazi kipya hapa nchini, Mflame wa Rhymes, Simba Mzee, Afande Sele akiwarusha vilivyo wakazi mbalimbali wa jiji la Mbeya, waliojitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa huduma mpya ya Airtel, Airtel Money uliofanyika jana jioni kwenye uwanja wa mpira wa miguu wa Sokoine.

Kundi la muziki wa kizazi kipya kutoka Temeke, Wanaume Halisi likiongozwa na kinara wao Juma Nature wakilishambulia jukwaa vilivyo jan jioni ndani ya uwanja wa Sokoine, kwenye uzinduzi wa huduma mpya itolewayo na kampuni ya simu ya mikononi ya Airtel, ijulikanayo kwa jina la Airtel Money.
No comments:
Post a Comment