Msaii wa hip-hop anafahamika zaidi kama Mwana  FA, sasa ameamua kuandika mashairi  yaliyotokana na wimbo wa taarab ambao  uliimbwa na wasanii wakongwe wa  muziki huo kutoka Tanzania Bara na  Visiwani. 
Staa huyo ambaye sasa anatamba na video ya Unanijua Unanisikia ameamua kumshirikisha msanii Linah kutoka THT ambaye naye kwa upande wake amesimama vilivyo katika nafasi hiyo.
Mwana FA alisema kuwa wimbo huo unafanana kabisa na zile nyimbo walizoimba wasanii wakongwe wa taarabu hapa nchini aliowataja kwa majina ya Siti Binti Saad, Malika pamoja na Bibi Kidude.
 Wimbo  huu kwenye chorus ameimba Linah na kurudia  kwa melodi ile ile na kisha  Mwana FA akaunganisha katika mashairi ya  nyimbo hizo. Gitaa limepigwa  na mmoja wa walimu wa muziki THT Cadinal  Gento na biti ameisimamia  Marco Chali kutoka MJ Records. Staa huyo ambaye sasa anatamba na video ya Unanijua Unanisikia ameamua kumshirikisha msanii Linah kutoka THT ambaye naye kwa upande wake amesimama vilivyo katika nafasi hiyo.
Mwana FA alisema kuwa wimbo huo unafanana kabisa na zile nyimbo walizoimba wasanii wakongwe wa taarabu hapa nchini aliowataja kwa majina ya Siti Binti Saad, Malika pamoja na Bibi Kidude.
No comments:
Post a Comment