Friday, October 14, 2011

Tunda Man fedha zangu nyingi zinaishia hotelini

Khaleed Ramadhan ‘Tunda Man’ aliyezaliwa Agosti 18, 1987 katika Hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam.Alianza kufuta ujinga mwaka 1994 katika Shule ya Msingi Makurumla, Magomeni jijini Dar es Salaam na baadaye aliendelea kupiga buku katika Shule ya Sekondari Forodhan. A-Level alisoma Sekondari ya Makongo, zote zipo Bongo.
Hayo ni kwa ufupi tu lakini mengi zaidi ungana nami kwenye maswali kumi hapa chini.

 Muziki ulianza lini na wimbo wako wa kwanza uliitwaje?
Tunda: Nilianza mwaka 2006 na wimbo niliotoka nao unakwenda kwa jina la Neila.

Hadi sasa ni mafanikio gani ambayo unaweza kujivunia kutokana na kazi zako za muziki?
Tunda: Mafanikio binafsi ni mengi ila kubwa zaidi ni kwanba nikifa nitazikwa na watu wengi sana.

Ni ugumu gani uliokumbana nao wakati unaanza kazi ya muziki?
Tunda: Katika kurekodi, maana sikuwa na fedha za kutosha hivyo ilinichukua muda kujipanga, sasa namshukuru Mungu kwa hapa nilipo.

Vipi kuhusu matumizi ya siku, unatumia shilingi ngapi?
Tunda: Chakula hunichukulia fedha nyinga sana, kwani sijui kupika kabisa hivyo ni lazima nile hotelini. Nateketeza si chini ya elfu thelathini kwa siku.

Sasa tuingie kwenye maisha yako ya kimapenzi, vipi una mpenzi?
Tunda: Ndiyo tena nampenda sana.

Vipi usumbufu kutoka kwa mademu micharuko?
Tunda: Usumbufu ni mkubwa sana lakini najua jinsi ya kukabiliana nao.

Ukiwa katika shoo za mikoani hupati vishawishi vya kumsaliti mpenzi wako?
Tunda: Mara nyingi huwa naambatana na mpenzi wangu kwa hiyo ni vigumu kumsaliti.

 Ukiwa chumbani na mpenzi wako ni jambo gani linakufurahisha zaidi?
Tunda: (Huku akicheka). Mpenzi wangu hupendelea kuvaa boxer yangu, hilo hunifurahisha sana.

 Duh! Je, huwa unapenda kumfanyia nini kabla ya mechi ya kiutu uzima?
Tunda: Mimi huwa sina mbwembwe faragha, ni burudani kwa kwenda mbele.

Utaoa lini maana umri naona unakuacha?
Tunda: Siku si nyingi nitafanya hivyo, sikilizieni tu.

No comments:

Post a Comment