Kuna kampeni ya kuhamasisha uchangiaji wa wananchi walioathirika na njaa kwenye pembe ya Africa na picha za wasanii maarufu kama Bob Marley na majina makubwa kwenye entertainment yametumika kwenye kampeni hiyo iliyobatizwa jina la Save the Children’s East Africa

Mtandao unaitwa www.imgonnabeyourfriend.org na ni lyrics zilizokuwamo kwenye track ya Bob Marley iitwayo High Tide or Low Tide ambayo imechaguliwa maalum na familia ya Bob Marley,na inakusudia kuwafikia watu milioni 1 kwenye Facebook na Twitter kupitia fans wao na documentary imetengenezwa kuonesha athari hiyo na director wa The Last King of Scotland,Kevin MacDonald

Kuanzia mwanzo wa wiki hii wasanii maarufu kama Lady Gaga,Justin Bieber,Beyonce,Eminem, Rihanna,Britney Spears,David Beckham,U2, Kanye West,Madonna,Jennifer Lopez,Muhammad Ali, Muse,Coldplay, Elton John,Lewis Hamilton,Bruno Mars,Cristiano Ronaldo,Sting wameanzisha kampeni kwa fans kupitia mitandao ya jamii ya Facebook na Twitter

Watu wapatao milioni 10 toka somalia na milioni 4 toka Kenya na ukanda wa Pembe ya Afrika wameathirika na njaa
No comments:
Post a Comment