Chuma Blog
Na: Luqman Maloto
Bila shaka wasomaji wangu mpo safi na mnaendelea na majukumu yenu kama kawaida. Tunaendelea kuanzia tulipoishia.
Dunia ilivyo ni kwamba huwezi kutoka kimapenzi na mtu halafu ikabaki kuwa siri. Iwe isiwe lazima itavuja. Japo maneno yanaweza yasifike kwa mumewe lakini kwa watu baki watamzodoa au kumsogoa kila anapopita.
“Yule ni mke wa mtu lakini tabia zake chafu”
Wapo watakaozungumza: “Yule mwanamke hana kinyaa, ana mume lakini utadhani changudoa kwa jinsi anavyoisaliti ndoa yake.” Wewe hutayajua hayo unayosemwa, utajiona upo vizuri ukiamini unayofanya hayaonekani. Kwa kudhani nyendo zako za siri hazijulikani, utawalaani machangudoa wanaojiuza mitaani.
Hapa namaanisha kuwa wakati tunawaweka sawa masistaduu, inapendeza lile kundi la wanawake wanaojiona wapo makini wakawa mfano wa kuigwa. Waache tabia za mafichoni, hadharani kujionesha ni watu wazuri kimaadili, wakati gizani wao ni wachafu kuliko hata hao wanaoonekana.
Japo natoa mifano mbalimbali, jambo muhimu kwako ni kutambua kuwa ninachokielekeza hapa ni somo kwamba kuna jamii fulani inapotosha tafsiri halisi ya mapenzi. Hii inasababisha maumivu makali kwa watu wanaoyaheshimu. Fikiria wewe unapenda, halafu upo kwenye uhusiano na yule asiyejua maana ya kupendwa.
Wewe unayaheshimu mapenzi na unayazingatia kwelikweli, hivyo unao utambuzi kwamba tafsiri ya kupenda ni kupendwa. Sasa upo kwenye uhusiano na mtu ambaye hajui kurudisha upendo kwa anayempenda. Anachoamini mapenzi ni mtindo huru, kama vile kwenda sokoni na kuchagua sehemu ya kununua bidhaa zako.
Tunaishi kwenye jamii moja, tunaona jinsi masistaduu na mabrazameni walivyochakachua mapenzi. Watoto wadogo siku hizi nao wanayatenda kama gemu. Tukielewana tunapeana leoleo. Alichoimba Ali Kiba kwenye Single Boy akimshirikisha Lady Jaydee, hakina tofauti na hali halisi iliyopo.
Kwamba hivi sasa hakuna mapenzi zaidi ya kudanganyana. Kwa hiyo, bora ukimpenda mmalizane leoleo. Hoja inayojengwa ndani ya wimbo huo ni kuwa mapenzi yanaumiza kichwa, unaweza kupenda sana matokeo yake ukawa kama mwendawazimu. Wanamaliza kila mmoja akijisifia alivyo singo.
Unaweza kuona wimbo huo kuwa maudhui yake yanalenga kuivuruga jamii kwenye suala zima la mapenzi. Kwa upande mwingine ni vizuri kupata wanafasihi kama Ali Kiba ili waichambue hali halisi kwa mtindo ambao ameuelezea na Jaydee kwenye Single Boy.

No comments:
Post a Comment