Chuma Blog
“Tunaipongeza
Serikali kwa kujipanga kurasimisha Sekta ya Sanaa lakini ni vema Sanaa
za Ufundi na Maonesho nazo zikahusishwa kwenye mchakato huu badala ya
filamu na muziki pekee” alishauri NKwama Balanga.

Mkuu
wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji kutoka Baraza la Sanaa la Taifa
(BASATA) Angelo Luhala (Katikati) akisisitiza jambo wakati akieleza
umuhimu wa Wasanii kujisajili ili kuwa tayari kwa ajili ya urasimishaji
wa Sekta ya Sanaa. Kulia ni Afisa Habari wa BASATA Aristides Kwizela na
Kaimu Mkuu wa kitengo cha matukio BASATA, Malimi Mashili.
Na Mwandishi Wetu
Baraza
la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka wasanii kujipanga kwa ajili ya
zoezi la urasimishaji wa sekta ya Sanaa linalotarajiwa kuanza ifikapo
Januari mwaka 2013.
Wito
huo umetolewa wiki hii na Mkurugenzi wa Idara ya Mfuko na Uwezeshaji,
BASATA Bw. Angelo Luhala wakati akitoa elimu kwa wadau wa Jukwaa la
Sanaa kuhusu ‘Urasimishaji wa Sekta ya Sanaa na Hakimiliki’ kwenye Ukumbi wa Baraza hilo ulioko Ilala Sharif Shamba
Alisema
kuwa, wasanii hawana budi kujipanga kuondoka kwenye mazingira ya
kufanya kazi kiridhaa na pasipokuwa rasmi bali wanyanyuke na waseme sasa
Sanaa ni kazi inayopaswa kupewa heshima yake kama kazi zingine.
“Wasanii
tuondoke kwenye ridhaa, tuseme Sanaa ni kazi kama zilivyo kazi zingine,
tuunge mkono jitihada za Serikali za urasimishaji sekta ya Sanaa
ifikapo mwezi Januari mwakani ili kuipa hadhi sekta hii” alisisitiza
Luhala.
Alizitaja
faida za urasimishaji sekta ya Sanaa kuwa ni pamoja na kazi zote za
Sanaa kutambuliwa kupitia kuwekewa stika maalum na mamlaka ya mapato
nchini (TRA) ili kudhibiti uharamia lakini pia kusaidia kupata takwimu
sahihi za sekta na kuchangia pato la taifa
“Kuanzia
Januari mwakani sekta hii itaanza kurasimishwa. Hii ina maana kuwa,
kazi za wasanii zitawekewa stika na TRA ili kudhibiti uharamia. Aidha,
mapato yatokanayo na Sekta ya Sanaa yatakuwa bayana kwa Serikali ili
kurahisisha upatikanaji wa takwimu na kupanga mipango ya maendeleo ya
Wasanii” aliongeza Luhala.
Alizidi
kueleza kuwa, zoezi la urasimishaji sekta ya Sanaa ambalo limekuwa
likipigiwa chapuo na wasanii wenyewe halitakuwa na maana kama wasanii
hawatajitokeza kwa nguvu zote na kuunga mkono juhudi za Serikali.
Mbali
na Wasanii, Luhala alizitaja kumbi za Sanaa na burudani, makampuni ya
ukuzaji sanaa (mapromota), vikundi vya Sanaa, studio za kurekodia muziki
na filamu, wachoraji ramani za majengo na wapigapicha kama wadau
wengine wanaotakiwa kurasimishwa kupitia kusajiliwa na kupewa vibali.
Kwa
upande wa wadau waliochangia mjadala huo walipongeza hatua hiyo ya
Serikali kuona umuhimu wa kurasimisha sekta ya Sanaa lakini wakahoji
zoezi hilo kugusa Sanaa za filamu na muziki pekee.
No comments:
Post a Comment