Wednesday, July 11, 2012

WAJANJA WA BUSH WAMLIZA TIMBULO

Chuma Blog

Nyota  wa muziki wa kizazi kipya Bongo, ALLY Timbulo  ‘Timbulo’ amepatwa na tukio la aina yake baada ya wajanja wa Bush kumliza  kamera  kubwa aina ya sonny  wakati wa  paty maalumu aliyoifanya mwishoni mwa wiki iliyopita  kijijini kwao Riuwa, Wilayani Mbalali jijini Mbeya.

Akizunguma na  Teentz mapema leo Timbulo  amesema  kuwa aligundua kupotea  ghafla kwa kamera yake hiyo mara baada ya kumalizika kwa paty hiyo iliyokuwa imechangamka kupita kiasi huku vijana wengi aliokuwa wamefurika  wakiwa  hoi kwa mitungi.
“Nilipomaliza kuimba  nikawa nimechili sehemu napumzika, lakini baada ya party kuisha  nianza kukusanya vitu vyangu na baadae nikagundua kuwa kamera yangu haipo, kwa kweli nilichanganyikiwa kwa kuwa  bado ni mpya kabisa na niliinunua kiasi cha dola 800 za Marekani” alisema  Timbulo
Akiendelea zaidi timbulo amesema kuwa juhudi za kumsaka mtu aliyesepa na kamera hiyo ya kisa bado zinaendelea kwa kuwa  sehemu kubwa ya watu waliofika siku hiyo wanafahamiana hivyo anaamini ndani ya siku chache zijazo atakuwa  ameipata.
 katika shoo hiyo Timbulo amerifu kuwa  jukwaa alilokuwa analitumia kuwaburudisha mashabiki wake  lilishindwa kuhimili vishondo  na kuvunjika  kufuatia  watu kushindwa  kuvumilia na kupanda juu alipokuwa yeye na hatimaye  jukwaa hilo likasalimu amri.
“Hakika ilikuwa siku mbaya kwani  kuna mambo mengi yalijitokeza ikiwamo shughuli yangu kucheleweshwa baada ya mchana na kuwa ucku kutokana na mtendaji  wa kata kuzuia mpaka diwani alipoingilia kati na kuniruhusu” alimaliza.

 STORI NA: DISMAS




 
 
 

No comments:

Post a Comment