Chuma Blog
SHINDANO
maalum lililotamba miaka nyuma la Maisha Plus, ambalo washiriki wake
hukaa kwa miezi miwili kijijini, linatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa
kushirikiana na shirika la Oxfam Tanzania, kupitia program yake ya ‘Mama
shujaa wa chakula’.
Akizungumza
kwa jana, Kiongozi Mtendaji wa kampuni ya DMB, Masoud Ali ‘Masoud
Kipanya’ alisema kuwa, shindano hilo la aina yake linakuja tena kwa
msimu wa tatu, likiwa na utofauti kabisa, huku mambo mbalimbali
yakiboreshwa, ikiwemo mshindi kuibuka na kitita cha sh milioni 20.
Kipanya
alisema kuwa, kwa kushirikiana na wadhamini wakuu, Oxfam Tanzania,
kupitia program yao ya ‘Mama shujaa wa chakula’, ambako watapata fursa
ya kuwaweka wanawake kwenye shindano, kwa kukaa ndani ya jumba hilo la
Maisha Plus huko kijijini kwa wiki mbili.
“Kwa
kushirikiana na Oxfam, shindano hili tumeborsha na litakuwa la aina
yake, ambapo washiriki watakaobahatika kushiriki, watafurahia na
watajifunza mengi na safari hii Mama shujaa wa chakula nao watabahatika
kukaa kwa wiki mbili, kisha watatoka na washiriki wa Maisha Plus
kuendelea na kinyang’anyiro cha kuwania kitita hicho cha milioni 20,”
alisema Kipanya.
Aidha,
aliwataka vijana wa kitanzania, kuchangamkia fursa hiyo, ambako
wanatarajia kuanza kufanya usaili mkoani Arusha, Agosti 3 na kisha
kuendelea kwenye mikoa mingine 14, ikiwemo ya Bara na viswani Zanzibar.
Pia,
alitoa wito kwa wadhamini wengine, kutumia nafasi hii kujitokeza ili
kupata kutangaza, kwani shindano hilo licha ya kufanyika misimu miwili
ya 2009 na 2010, huku 2011 likishindwa kufanyika kutokana na kukosa
udhamini, limejizolea sifa na kupendwa na watu wa rika mbalimbali.
No comments:
Post a Comment