Chuma Blog
Msanii mkongwe nchini Dudu Baya anadaiwa kumpiga mtangazaji wa kituo
cha radio cha Kiss FM Ezden chenye makao yake jijini Mwanza, Ezden
Jumanne aka The Rocker.
Akiongea kwa simu na Bongo 5, Ezden amesema issue ilianza kabla ya
ijumaa iliyopita ambapo alikuwa ameandaa show iitwayo Mwanza Blast
iliyoendana na uzinduzi wa mixtape ya rapper Nash MC iitwayo ‘Mzimu wa
Shaaban Robert’.
Amesema baada ya Dudubaya ambaye kwa sasa yupo Mwanza kuona matangazo
ya show hiyo alianza kuponda mtaani kuwa show hiyo haina maana na
‘itakula za uso.’
Ezden amesema kitendo cha yeye kutomjumuisha kwenye roaster ya waliopanda kwenye show hiyo kilimuuma.
Dudu Baya aliamua kumtafuta Dj John wa Radio Free Africa kumuomba
nafasi ya kupanda kwenye stage ya show hiyo kwa malipo kiduchu lakini
alikataa na kumwambia amtafute Ezden kwakuwa yeye ndio mwamuzi wa kila
kitu.
No comments:
Post a Comment