Tuesday, June 5, 2012

Bongo Star Search kuanza ziara ya Kusaka vipaji mkoani Dodoma June 15

Chuma Blog


ZIARA ya kusaka vijana watakaoshiriki katika shindano la Epiq Bongo Star Search
mwaka huu inaanzia mkoani Dodoma Juni 15 katika Ukumbi wa Royal Village.

Akizungumzia
ziara hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Benchmark Production Ritha
Paulsen alisema kuwa washiriki wanatakiwa kufika katika ukumbi huo
kuanzia saa 12 asubuhi.

Alisema kuwa
kampuni yake inatarajia kuchukua vijana watatu hadi watano kutoka mkoa
huo watakaouwakilisha mkoa huo katika fainali zitakazofanyikia Dar es
salaam.

Alisema kuwa wakiwa mkoani
humo wanatarajia kuona vipaji vya wasanii wa kila aina kwa kuwa EBSS
inalenga kukuza vipaji vya vijana wenye uwezo wa kuimba aina zote za
nyimbo.

“ Kama ambavyo imeshafahamika
kuwa mwaka huu mshindi wa EBSS atapata kitita cha shilingi milioni 50
taslim hivyo ni kwamba tunawaomba wakazi wa mkoa wa Dodoma wenye vipaji
kuja kwa wingi siku hiyo” alisema Ritha

Ritha ataongozana na majaji wengine ambao ni Salama na Master Jay.

No comments:

Post a Comment