Chuma Blog


Ndugu zangu,
Nimehuzunishwa
na picha za Mahakamani kwenye magazeti ya jana zikimwonyesha msichana
Elizabeth ' Lulu' Michael akilia hadharani.
Nikivaa
miwani ya mzazi nilimwona mtoto ambaye angeweza kuwa wangu. Nilimwona
mtoto anayedhalilishwa mbele ya macho ya jamii. Nilimwona mtoto
anayehukumiwa na jamii ambayo hadi sasa haijui ukweli wa kilichotokea.
Jamii
inapaswa kujiuliza, kwa nini picha za Lulu akiwa analia zina umuhimu
kwa wanajamii kuziona?Je, ni kwa sababu machozi ya Lulu ni dhahabu kwa
wengine? Kwamba yanasaidia kwenye kuuza magazeti? Je, kuwa na huzuni na
kutoa machozi si haki ya hisia za mwanadamu ambazo zinapaswa
kuheshimiwa? Kwa nini ziwekwe hadharani? Hicho ndicho jamii inataka
kukiona? Na ikishaona?
Tatafakari na:
Maggid Mjengwa,
Iringa.

No comments:
Post a Comment