Friday, April 6, 2012

Kilimanjaro Music Awards 2012 kufanyika April 12 ndani ya Mlimani City

Chuma Blog
Kampuni ya Bia


Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Kiliminjaro Prenium Lager kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) leo wametangaza rasmi tarehe ya usiku wa kutoa Tuzo za Muziki Tanzania (Kilimanjaro Tanzania Music Award).
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam ,Meneja wa bia ya Kilimanjaro Bwana George Kavishe alisema tarehe ya siku ya kutoa tuzo hizo ni tarehe 12 april 2012 ndani ya ukumbi wa Mlimani City.
“Shughuli itaanza rasmi saa moja jioni ikipambwa na burudani safi ilipangwa kwa umahili na mtaalam kutoka nyumbani. Wasanii watakaopanda usiku wa kutoa tuzo ni pamoja na Diamond, kundi zima la Tmk Wanaume, Charles Baba, Khalid Chokoraa, Recho, Ommy Dimpoz, Bichuka na wengine wengi” alisema Kavishe.
Aliendelea kusema, tamasha litakuwa kali kwani sio tu waitaimba nyimbo zao lakini wataimba na nyimbo za zamani zilizowahi kutamba enzi za wanamuziki nguli nchini.
Pia meneja wa Kilimanjaro ametoa shukrani kwa Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kupiga kura. “Tumevuka lengo la idadi ya kura kwa Nyanja zote ni maana ya ujumbe mfupi wa simu, vipeperushi, barua pepe na mitandao hii imaanisha Tuzo za zimekubalika na zimepokelea na jamii”.
Aidha aliendeleakutoa shukrani kwa BASATA kwa kuendelea kutoa ushirikiano na kampuni ya TBL kupitia bia ya Kilimanjaro na kuipatia tena kibali cha kudhamini na kuendeleza shughuli za Tuzo za Muziki Tanzania.
Tiketi zitauzwa kwa kwa VIP shilingi elfu 75 ikijumuishwa na chakula cha jioni (Buffet) na vinywaji bure, na kawaida zitauzwa kwa shilingi elfu 20, na bia moja ya bure.
Tiketi zitauzwa maeneo ya Ukumbi wa Mlimani City kuanzia Jumatatu, Posta Mpya ‘Baraka Golden mtaa wa Azikiwe nyuma ya CRDB Bank’, Zizzou Fashion ya Victoria, Sinza na Tegeta, Born To Shine Mwenge, Robby One Fashion Kinondoni, Engine Petrol station Mbezi.

No comments:

Post a Comment