Wednesday, April 11, 2012

FELLA AKAMATWA NA POLISI SIKU YA PASAKA NA KUPELEKWA SELO

Chuma Blog
 Baada ya Fella kufikishwa katika kituo cha Polisi Morogoro
Fella akiingizwa Selo
 Ni siku ya Pasaka ambapo Mkubwa na Wanae wakiwa katika show mjini morogoro,ambapo walifika mapema sana na kuanza show katika kiwanja cha jamhuri.
Show ikiwa inaendelea na wasanii wakiwa wanafanya kweli na kuwafanya mashabiki kuwa na furaha ya Pasaka.Ratiba ya show ilikuwa inasema kuwa show itaanza muda wa mchana na kumalizika 12 jioni.kwani ilipofika muda jioni polisi walikuwepo katika eneo la kiwanja na kujisogeza karibu ya deejay.
Wasanii wakiwa jukwaani wakiwa wanaendeleza burudani bila ya kujuwa muda wa kibali umekwisha na kama kawaida ya Fella akiwa karibu ya Dj akiwa anatowa maelekezo ya nyimbo za kupigwa kwaajili ya wasanii wake.Alisogea polisi mmoja na kumwambia kuwa muda umekwisha wa kufanya show na ndipo Fella ikambidi kumwambia polisi kuwa kutokana na mvua kunyesha tumechelewa kuaza show,ila polisi yule akawa ameelewa.
Kukaa muda si mrefu alitokea polisi mwingine na kujitambulisha kwa fella yeye anaitwa "Sheih kihondo mkuu wa kituo cha polisi Morogoro" na kumuamulu polisi mwingine akamkate Fella na kumpeleka kituo cha polisi..........

No comments:

Post a Comment