Chuma Blog

Msanii wa zamani wa
Kundi la Mexicanna La Cavera, Baghdad, leo amesema yeye yuko tayari
kufikishwa mahakamani ama mbele ya mkondo wa sheria na wasanii wenzake
waliobakia kwa kuwa yeye anayohaki ya kumiliki na kutumia nembo ya
Mexicana kibiashara.Akiongea
kwenye kituo kimoja cha Radio Mwishoni mwa wiki ,Baghdad
alikuwa akijibu tuhuma ambazo ziko mtaani kuhusu mtafaruku na mtifuano
kati ya wasanii hao ambapo msanii alisema yeye ndiye alilipia “Plates”
ama sahani zinazotumika kuchapa nembo mbali mbali.“
Mimi ndiye niliyelipia plates hizo na baada ya msanii Baghdad kujitoa
sisi hatukumchukulia hatua za haraka haraka kumdai vitu vya Mexicanna La
Cavera kwa sababu alikuwa anaumwa sana. Baadae tulipomfuatilia Baghdad
tukaona ameanza kutumia nembo yetu kwenye mtandao wa Facebook akinadi
fulana zake’, alisema mmoja wa wasanii wa kundi hilo.....Baghdad alimaliza kwa kusema,’Siongei na mshika kamba mbwa bali naongea na mwenye mbwa mwenyewe’.Sasa bado haijajulikana kwa jinsi utata huu ulivyo ni nani mwenye mbwa ama mmiliki halali wa kundi hilo...
No comments:
Post a Comment