Thursday, February 23, 2012

SHETTA’ KUACHIA NGOMA YA “NIDANGANYE”

Chuma Blog
BAADA ya kufanya vizuri na ngoma yake ya ‘Mdananda’, msanii Shetta, anatarajia kuachia kitu kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Nidanganye’, akiwa amemshirikisha Diamond kipenzi cha warembo. Shetta alisema kuwa kazi hiyo itakuwa ni moto mkali kwani anaamini baada ya kushika soko na ngoma yake iliyopita hiyo itakuwa zaidi.

Alisema kuwa ameamua kumshirikisha
Diamond, katika wimbo huo ni kutokana na uwezo mkubwa aliyokuwanao hivyo anaamini sauti yake itaweza kuifanya ngoma hiyo kulikamata soko kikamilifu.

Aliongeza kuwa baada ya mchakato wa wimbo huo, atakuwa katika maandalizi ya albamu yake ya pili ambayo bado hajaipa jina huku akiaamini itafanya vizuri.


“Kwa sasa nupo katika hatua za mwisho wa kumalizia ngoma yangu hiyo, hivyo nawaomba mashabiki wangu wakae tayari kuipokea,”
alisema.

Na Laurent Samatta

No comments:

Post a Comment