Thursday, December 29, 2011

Wakazi wa Mbagala wakumbukwa kwa ukumbi wa kisasa

Lango la kuingilia Dar Live
Ndege ya Dar Live iliyoko ndani ya ukumbi kwa ajili ya watoto
Jukwaa likijengwa katika kiwanja hicho.

Ukumbi mpya wenye hadhi ya kimataifa wa Dar Live uliopo Mbagala jijini Dar es Salaam unatarajiwa kuzinduliwa rasmi Januari Mosi, 2012 na kusindikizwa na burudani ya nguvu kutoka kwa wasanii kibao wakiongozwa na Juma Kassim Kiroboto ‘Sir Nature’ sambamba na Kundi la Muziki wa Kizazi Kipya la Gangwe Mob. Nature, Haroun Kahena ‘Inspekta’ na mwenzake Karama Bakari ‘Luteni Kalama’ wameahidi kuonesha ukongwe wao katika gemu na kuandika historia ya kipekee kwa kuangusha bonge la shoo ya uzinduzi, ambapo watakamua steji moja na Mzee Yusuph atakayekuwa na kundi zima la Jahazi Modern Taarab bila kuwasahau Extra Bongo chini ya Ali Choki ‘Mzee wa Farasi’. “Kama bado ulikuwa unaamini kuwa Mbagala ipo nyuma kwa burudani za kimataifa, basi umechelewa kujua kwani Mwaka Mpya ndiyo siku ambayo Wabongo watajionea wenyewe maujanja yanayopatikana ndani ya Dar Live! Haya ni mapinduzi katika tasnia ya burudani,” alisema Nature.

No comments:

Post a Comment