Friday, September 16, 2011

THT KUSHEREHEKEA MAHAFALI YA SITA KWA VIJANA WAKE 30 WANAOMALIZA MAFUNZO YA MUZIKI




Taasisi isiyo ya Kiserikali, THT inatarajia kufanya mahafali ya sita kwa vijana wake 30 wanaomaliza mafunzo ya muziki,hafla hiyo itakayokuwa ya aina yake itafanyika Septemba 18,2011,siku ya jumapili.

Hafla hiyo itakayojumuisha wageni waalikwa na wadau mbalimbali wakiwemo na wasanii kadha wa kadha, itafanyika maeneo ya Morocco Block 41 nyuma ya mgahawa wa Bestbite ambako ndiko kwenye tukio husika la THT.


Aidha kabla ya kupewa vyeti vyao,wahitimu hao watatoa burudani LIVE kuonesha nini hasa wamejifunza takribani mwaka mmoja,kama vile haitoshi panapo Wahitimu hapakosi kuwapo na Wakongwe,hivyo wahitimu hao watajumuika na wasanii waliotangulia na waliopita THT kutoa burudani murua kabisa kwa wageni waalikwa watakaofika.


“Tunawashukuru sana waliotuunga mkono kwa kipindi hiki,hata kufikia lengo hili.Wapo wadau wetu ambao wamekua wakitupa kazi mbalimbali ili kutuwezesha kumudu mahitaji yetu ya kila siku kwa ujumla,ama kwa hakika kwa Watu hawa hatuna neno zuri zaidi ya kusema ASANTE na TUNAWASHUKURU sana”.


Kama vile haitoshi pia tunawapa pole sana waliofiwa na ndugu zao katika ajali ya meli Zanzibar. MUNGU AZILAZE ROHO ZA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI AMEN.


Michael Nkya.

Mratibu,

No comments:

Post a Comment