Mchekeshaji wa longtime bongo, ambae amekua akitumika kwenye majukwaa ya siasa kutokana na ukali wake wa kuigiza sauti za viongozi mbalimbali, Steve Nyerere ameamplfy kwamba ametumia Milioni 25 za kibongo katika kuiandaa movie mpya, inayoonyesha maisha aliyoyapitia mpaka kufika alipo president Jakaya Kikwete.
Movie imetengenezwa kwa mwezi mmoja, na gharama yake imekua milioni 25 kwa sababu ni movie iliyohusisha watu wengi, wametumia location mbalimbali za gharama, ikiwemo bagamoyo nyumbani kwa president, ukumbi wa Bunge, misafara ya rais ambayo ina magari ya kifahari, pikipiki, Ambulance, imetumika pia nyumba inayofanana na ikulu.
Steve Nyerere akiongea na millardayo.com amesema japo amewahi kukutana mara kadhaa na rais Ikulu, bado hajamfahamisha kwamba amecheza movie inayohusiana na maisha yake.
Movie itaanza kuuzwa rasmi pale Moven pick hotel dec 3 2011 na cd zitaanza kuuzwa hapohapo.habari na millard ayo
No comments:
Post a Comment