Thursday, August 18, 2011

FFU wa Ngoma Africa Band kutingisha Jukwaa Ujerumani

 Kutingisha Jukwaa la Afrika Festival,Aschweiler,Ujerumani
Jumamosi 20.08.2011
 
"Mzimu wa muziki wa dansi unaendelea kuwabangua vichwa washabiki ughaibuni !"
 
 
Bendi Maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU,
wanatalajiwa kutumbuiza katika onyesho lingine kubwa la wazi mjini Aschweiler,nchini
Ujerumani siku ya jumamosi 20.08.2011 saa 12.00 jioni.
 
Maporomota wa muziki huko ughaibuni wamehamua kuifanyia kweli bendi hiyo maarufu kwa
kuipangia ratiba ya maonyesho bila kupumua !
Ras Makunja na kikosi kazi chake Ngoma Africa band aka FFU wamejikuta wapo katika
kibarua sugu cha kuwapa burudani kamili wapenzi wa muziki katika kila kona huko ughaibuni.
FFU kw sasa wanatamba na nyimbo mbili mpya "Bongo Tambarare " na "Supu ya Mawe"
wasikilize at www.ngoma-africa.com

No comments:

Post a Comment